Mazonge

Wee nipende hivyo hivyo mama
Japo mambo ndivyo sivyo mama
Punguza na masikitiko sana
Tupendane mpaka kifo mama

Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh

Jana tumelala njaa
Paka amelala jikoni
Kibanda chetu chavujaa
Usiku tunalala kihunii

Ulisema utanipenda mpaka mwisho
Hutonikimbiaa yaaah
Na hali yangu ni ngumu mahangaiko
Utavumilia yaah

Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh

Mbona nayona mengi natamani
Lakini natuliza moyooo
Japo wanasema mengi majirani
Napuuza naachana nayooo
Mwenye nacho anaongezewa (eeeh)
Urefu wa kamba nasubiria
Bila Imani utanikimbia mpenzi
Kwa hii hali nachechemea

Shilingi yaua mume wangu
Mlinzi nalinda pendo langu
Japo kidogp ndo cha kwangu
Mungu anajua kesho yangu
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Baba oohh
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Baba oohh

Nakupenda hivyo hivyo Baba
Japa mambo ndivyo sivyo Baba
Hata na mahangaiko hayaaa
Ntakupenda mpaka kifo Baba
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Baba oohh
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Baba oohh

Kazi nimefukuzwa
Kibarua kimeota nyasi mamaa
Joto lanifukuta
Mfukoni sina hata hela ya ngama
Nasikia mama mwenye nyumba nae
Anataka kodi yake
Hivi kweli
Mazonge yamepitilza
Na sipati jibu lake saa nafeli
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh
Aah eeeh... Aaah eeh
Aaah eeh, Mama oohh

Piga konde baba
Kidogo ndo ujaza kibabaa
Ridhiki mafungu saba
Tunachopata tushukuru si haba
Ukweli kusema nakupenda tu
Sijari kwa hali iwe chini ama juu
Wao kwa magari sisi kwa miguu
Tule kachumbali miguu ya kuku (Huuu huuu)
Mkono mtupu haulambwi baby
Utanipenda vipi
Penzi tupu bila pesa halitambi
Utanielewa vipi
Nimeamini kweli wee kipenda roho
Na nyama mbichi imenikaba koo
Tule kipolo (aaah eh)
Giza totoro (yaa wee)

Uuh mama yee ... mh
Wee chaguo langu
Wee baba wee… Wewe mwandani wangu
Nitakupenda milele... Unipende milele
Nitakupenda milele... Unipende milele
Iyee iyee iyee...
Aah eeh aah eeh
Uuh uuh

Most popular songs of Bright

Other artists of Pop rock