Atarudi

Na ye ni mwanadamu, Na dunia tunapita
Kama kupata kwa zamu, Oh zamu, yangu itafikaa
Siwezi kana damu, Kesho wataja nizika
Ila ningependa afahamu, Haya mateso aloniipa

Mmh! Tena mwambieni aloninyima mimi, ndio kampa yeye eh
Kupata foleni, Nasubiri yangu mimi, Hata ichelewe eh

Oh Oh Oh
Sina furaha naigiza ilimradii, Watoto wasijihisi vibaya
Huyu mdogo anauliza Eti Daddy, Mama ameihama kaya
Cha kujibu sina nabaki tu kusemaaaaa

Atarudi, atarudi mama
Atarudi, anawapenda sana
Atarudi, atawaletea zawadi
Atarudi, eh atarudi mama
Atarudi, atarudi mama
Atarudi, anawapenda sana
Atarudi, atawaletea zawadi
Atarudi

Siwezi sema sijui tatizo, Hali yangu duni imefanya ukanikimbia
Ni vyema ungefanya maigizo, Mara kumi usingenizalia
Mmmh, Ingali Mapenzi pekee, Ningesema ni changamoto nijifunze
Ameniacha mpweke, Na watoto niwatunze
Eh, Ila siwezi laumu (Ah), Wenda yupo sawa (Ah)
Kipato changu kigumu (Ah), Kutwa Bumunda na Kahawa (Ah)

Eh! Ila mwambieni aloninyima mimi, Ndio kampa yeye eh
Kupata Foleni, Nasubiri yangu mimi, Hata ichelewe

Oh Oh Oh
Sina furaha naigiza ilimradi, Watoto wasijihisi vibaya
Huyu mdogo anauliza Eti Daddy, Mama ameihama kaya
Cha kujibu sina nabaki tu kusema

Atarudi, atarudi mama
Atarudi, anawapenda sana
Atarudi, atawaletea zawadi
Atarudi, eh atarudi mama
Atarudi, atarudi mama
Atarudi, anawapenda sana
Atarudi, atawaletea zawadi
Atarudi

(Oh My God It's Beta Sound)

Most popular songs of Harmonize

Other artists of Afrobeats