Ntarejea

Vipi mizigo umeshaweka tayari
Sijechelewa nkaachwa na gari
Basi jikaze usilie mpenzi
Mi nitarudi niombee kwa mwenyezi
Zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna
Huwa nakosa raha pale mkikosa cha kutafuna
Roho yangu inauma, sema ntafanya nini na pesa sina
Nakuonea na huruma, bora niende mjini kusaka Tumaa

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
Nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea

Wanajua kwamba nafsi na roho vitakuwa na wasiwasi
Ukumbuke na moyo utajawa na simanzi
Ntakapokuwa nakwenda shambani afu niko peke
Yangu honey
Ntapokuja kuwa na majirani ntaumia aaah
Pale napotoka kisimani ama nipo na kuni kichwani
Sina wakunitua nyumbani ntaliaa

Maneno yako yananfanya nakosa raha na mawazo
Hata mwenzako sijawahi kufika dar huu ndo mwanzo
Vile nakwenda na sijui pa kukaaa wala mavazi ooh
We niombee niepushwe na balaa na maradhi ooh

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
Nawe usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea

Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na Sisi
Usisahau kama mkeo na wana, umetuacha na dhiki
Vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na Marafiki
Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie Sidanganyiki

Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na Sisi
Kumbuka mkeo na wana nyumbani, umetuacha na Dhiki ooh
Vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na Marafiki
Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie Sidanganyiki

Ntarejea mama
Niombee nirudi salama
Ohhh watoto wadanganye
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
Wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
Nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea

Most popular songs of Diamond Platnumz

Other artists of Electro pop